Zaburi Chapter 129
1
Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa,
2
Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza.
3
Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao.
4
Bwana ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki.
5
Na waaibishwe, warudishwe nyuma, Wote wanaoichukia Sayuni.
6
Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea.
7
Ambayo mvunaji haujazi mkono wake, Wala mfunga miganda kifua chake.
8
Wala hawasemi wapitao, Amani ya Bwana ikae nanyi, Twawabariki kwa jina la Bwana.