Zaburi Chapter 4
1
Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Umenifanyizia nafasi wakati wa shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu.
2
Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo?
3
Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa; Bwana atasikia nimwitapo.
4
Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
5
Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana.
6
Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema? Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
7
Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
8
Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.