Zaburi Sura 67
1
Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake.
2
Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote.
3
Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.
4
Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
5
Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.
6
Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu wetu, ametubariki.
7
Mungu atatubariki sisi; Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.