Isaya Chapter 12
1
Na katika siku hiyo utasema, Ee Bwana, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.
2
Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.
3
Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
4
Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litajeni jina lake kuwa limetukuka.
5
Mwimbieni Bwana; kwa kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya katika dunia yote.
6
Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.