Zaburi Sura 113
1
Haleluya. Enyi watumishi wa Bwana, sifuni, Lisifuni jina la Bwana.
2
Jina la Bwana lihimidiwe Tangu leo na hata milele.
3
Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa.
4
Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote, Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5
Ni nani aliye mfano wa Bwana, Mungu wetu aketiye juu;
6
Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani?
7
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8
Amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake.
9
Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.