Zaburi Sura 114
1
Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2
Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake.
3
Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma.
4
Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo.
5
Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma?
6
Enyi milima, mruke kama kondoo waume? Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7
Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana, Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.
8
Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi.