Zaburi Chapter 120
1
Katika shida yangu nalimlilia Bwana Naye akaniitikia.
2
Ee Bwana, uiponye nafsi yangu Na midomo ya uongo na ulimi wa hila.
3
Akupe nini, akuzidishie nini, Ewe ulimi wenye hila?
4
Mishale ya mtu hodari iliyochongoka, Pamoja na makaa ya mretemu.
5
Ole wangu mimi! Kwa kuwa nimekaa katika Mesheki; Na kufanya maskani yangu Katikati ya hema za Kedari.
6
Nafsi yangu imekaa siku nyingi, Pamoja naye aichukiaye amani.
7
Mimi ni wa amani; Bali ninenapo, wao huelekea vita.