Zaburi Sura 122
1
Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.
2
Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.
3
Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana,
4
Huko ndiko walikopanda kabila, Kabila za Bwana; Ushuhuda kwa Israeli, Walishukuru jina la Bwana.
5
Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.
6
Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao;
7
Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
8
Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe.
9
Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu, Nikutafutie mema.