Zaburi Sura 127
1
Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.
2
Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
3
Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu.
4
Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani.
5
Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni.