Zaburi Sura 126
1
Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto.
2
Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu.
3
Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi.
4
Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini.
5
Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.
6
Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.