Zaburi Chapter 125
1
Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.
2
Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.
3
Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.
4
Ee Bwana, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo.
5
Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, Bwana atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.