Zaburi Chapter 124
1
Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa,
2
Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia.
3
Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu
4
Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu;
5
Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo.
6
Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.
7
Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.
8
Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.