Zaburi Sura 149
1
Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.
2
Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.
3
Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie.
4
Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
5
Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
6
Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.
7
Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu juu ya kabila za watu.
8
Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, Na wakuu wao kwa pingu za chuma.
9
Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote. Haleluya.