Zaburi Sura 70
1
Ee Mungu, uniokoe, Ee Bwana, unisaidie hima.
2
Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.
3
Warudi nyuma, na iwe aibu yao, Wanaosema, Ewe! Ewe!
4
Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu.
5
Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Bwana, usikawie.